Ibn Khaldun Learning Academy
Watch Video
Dumisha uwiano wa akili, mwili, na roho.
Ushirikishwaji ndio nguvu yetu. Daima jitahidi kuwa bora zaidi.
Fanya dunia iwe mahali bora pa kuishi.

Kuhusu IKHLA

Karibu kwenye kitovu cha elimu yenye mabadiliko, mahali ambapo maarifa yanakutana na maadili! IKHLA imejitolea kujenga mustakabali bora kwa kulea wanafikra makini, kuzalisha viongozi waadilifu, na wanafunzi wa maisha yote. Ingia katika mazingira ya kujifunza yenye uhai yanayochochea hamu ya kujua, ubunifu, na maendeleo ya tabia.

Dira Yetu

Kua kwa maarifa! Kuwa kiongozi imara mwenye moyo mwema.

Kwa Nini IKHLA?

Tumedhamiria kukutanisha maarifa yanakutana na maadili kwa mustakbali mwema wa jamii.

Msingi Wetu

Dumisha uwiano wa akili, mwili, na roho.

Muundo wa Taasisi

Muundo wetu wa taasisi umeundwa kuhakikisha utendaji bora na uwazi wa majukumu kwa kila idara.

  • Bodi ya Wadhamini – Husimamia mwelekeo wa kimkakati.
  • Uongozi wa Utendaji – Unahusika na usimamizi wa kila siku.
  • Vitengo vya Programu – Vinatoa mafunzo, tafiti na huduma za kijamii.
  • Washirika wa Maendeleo – Hutoa msaada wa kifedha na kiufundi.
Organization Structure

Muundo huu unaonyesha uhusiano wa kiutawala kati ya Bodi ya Wadhamini, Uongozi wa Taasisi, Idara mbalimbali, na vitengo vya utekelezaji wa miradi ya kielimu na kijamii.

Ujumbe kutoka kwa Principal & CEO – Ibn Khaldun Learning Academy (IKHLA)

Karibu sana Ibn Khaldun Learning Academy (IKHLA) – Kitovu cha maarifa, maadili, na maendeleo ya kijamii.

Katika dunia inayobadilika kwa kasi, tunaamini kwamba elimu si tu chombo cha mafanikio binafsi, bali ni mwangaza wa jamii na kizazi kizima. Hapa IKHLA, tunajivunia kuwa sehemu ya safari hii muhimu, tukiwalea vijana na watu wazima kuwa viongozi wa kesho wenye ujuzi, maadili, na maono makubwa.

Kwa kupitia idara zetu mbalimbali, tunatoa:

  • Mafunzo ya kitaaluma na kiufundi kwa walimu, wanafunzi, na wajasiriamali.
  • Programu za lugha (Kiingereza, Kiarabu, na Kiswahili kwa wageni).
  • Mafunzo ya teknolojia kwa karne ya 21.
  • Mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi.
  • Semina elekezi kwa wahitimu wanaojiandaa na vyuo na maisha ya kitaaluma.
  • Huduma za kijamii na kuimarisha maadili kupitia miradi mbalimbali kwa jamii.

Kwa kushirikiana na washirika wetu ndani na nje ya nchi, tunajitahidi kutoa elimu inayogusa akili, moyo, na maisha ya kila mshiriki wetu. Tunaamini katika elimu inayowezesha mtu kufikiri kwa kina, kuishi kwa maadili, na kutenda kwa ubunifu.

Tunakualika kuwa sehemu ya familia ya IKHLA.
Pamoja, tuwalee kizazi cha mabadiliko!

Kwa heshima kubwa,
Said A.S. Yunus
Principal & CEO
Ibn Khaldun Learning Academy (IKHLA)

Our Location