Kuhusu Programu ya EDK

Programu ya Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK) ni mradi maalumu ulioanzishwa chini ya Taasisi ya IKHLA kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu katika skuli za Zanzibar ambapo kwa sasa umeanza katika Wilaya ya Wete kwa skuli ambazo zipo Wete Mjini. Programu hii ilianzishwa rasmi tarehe 26 Januari 2022, kufuatia changamoto za ufaulu mdogo, ukosefu wa mbinu bora za kujifunzia, na mmomonyoko wa maadili ya wanafunzi. Kwa kutumia mfumo wa ushindani wa kitaaluma kati ya wanafunzi na skuli, EDK inalenga kuongeza ufaulu wa somo hili, kukuza maadili ya Kiislamu, kupunguza idadi ya wanafunzi wa division zero, na kuimarisha ushirikiano kati ya walimu, wazazi, na taasisi za elimu ya Kiislamu.

Malengo ya Programu

  1. Kuboreshwa kwa ufundishaji wa Elimu ya Dini ya Kiislamu.
  2. Kupunguza division zero katika somo hili.
  3. Kukuza maadili ya Kiislamu miongoni mwa wanafunzi.
  4. Kuongeza hamasa kwa wanafunzi na walimu kuhusu umuhimu wa somo.
  5. Kuimarisha ushirikiano baina ya skuli, walimu, wazazi na taasisi za Kiislamu.

Maendeleo ya Programu

Tangu kuanzishwa kwake

  1. Mwaka 2022, skuli 4 zilishiriki.
  2. Mwaka 2023, skuli 5 zilishiriki.
  3. Mwaka 2024, idadi zimeongezeka hadi skuli 7.

EDK imeleta matokeo chanya, ikiwemo:

  1. Kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi.
  2. Kuimarika kwa maadili na nidhamu.
  3. Kuboreka kwa mbinu za ufundishaji.
  4. Ushirikiano mkubwa zaidi kati ya walimu, wazazi, na taasisi zinazosaidia elimu ya Kiislamu.

Mafanikio

  1. Ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa kiwango kikubwa.
  2. Wanafunzi wamepata mwamko mpya wa kujifunza na kuelewa somo.
  3. Maadili mema yameimarika katika jamii na mashuleni.
  4. Walimu wamepata mafunzo maalum na mbinu bora za kufundisha.

Changamoto

  1. Uhaba wa vitabu vya rejea na rasilimali za kujifunzia.
  2. Ukosefu wa walimu wa kutosha waliobobea katika somo hili.
  3. Upungufu wa fedha za kuendesha programu kwa ufanisi.
  4. Changamoto ya baadhi ya wanafunzi na jamii kutoona umuhimu wa somo hili.

Wito kwa jamii

Kwa mafanikio haya makubwa ndani ya kipindi kifupi, tunatoa wito kwa jamii nzima kushirikiana nasi kwa hali na mali, ili kuhakikisha kuwa kizazi kijacho kinaendelea kupata elimu bora ya Dini ya Kiislamu. Ushirikiano wenu ni msingi wa mafanikio ya programu hii.

Ripoti

Bonyeza hapa kupakua ripoti ya EDK